Mnamo tarehe 17/09/2014 jumatano abiria kutoka kahama wagomea gari la Bedui ambalo lilikuwa linaenda kigoma leo ahsubuhi.
Abiria wakichuku mizigo yao baada ya gari hilo kuharibika njiani. Wakina mama, watoto, vijana pamoja na wanafunzi walienda moja kwa moja polisi kushtaki hilo gari kwa lengo la kurudishiwa pesa zao.
Kwa msaada wa maaskari wa kahama, ufumbuzi ulipatikana japo kulikuwa na uvutani kati ya maagenti wa kwenye gari na abiria. Baada ya maasaa manne, pesa zilirudishwa na abiria wakajumuhika kukodisha gari lingine ili liwapeleke hadi kigoma. Mnamo saa tano walipata gari lingine na kuanza safari yao.
Yaani, ingekuwa huu ushirikiano upo kila mahali, watu wangewajibika sana katika nyazfa zao.